Wednesday, April 26, 2017

Waunguza wangu moyo



Ewe bin fulani,mbona wanipa madhila?
Wanitesa jameni,wapi umetoa hila?
Nimekuweka rohoni,waniwacha kwa jalala
Waunguza wangu moyo,habibi hilo jua

Nikikumbuka zamani,machozi tilalila
Huba ile haifanani,furaha majonzi bila
Tukaingia ndoani,iliyopangwa na mola
Waunguza wangu moyo,habibi hilo jua

Rejelea ya zamani,nakua si wa kulala
Unanijia ndotoni,hata lepe sijalala
Sema warejeani,moyo wangu haujala
Waunguza wangu moyo,habibi hilo jua

Nikikutia mbonini,yatayeyuka madhila
Nitakubusu mdomoni,bila aibu wala
Nifungie pembejoni,hiyo ndio yangu swala.
Tafurahi si kifani, habibi hilo jua


Na Hafifa Bahfif

No comments:

Post a Comment